9 Aprili 2015 - 19:02
Idadi ya waliouwawa yaongezeka Kenya

Idadi ya watu waliouwawa katika shambulio la kigaidi wiki iliyopita dhidi ya chuo kikuu nchini Kenya imepanda na kufikia 152.

Idadi  ya  watu  waliouwawa  katika  shambulio  la  kigaidi  wiki iliyopita  dhidi  ya  chuo  kikuu  nchini  Kenya  imepanda  na  kufikia 152.

Msemaji  wa  wizara  ya  mambo  ya  ndani Mwenda Njoka amesema  leo  kwamba  idadi  hiyo  inabadilika  kila  mara  hadi  pale miili  yote itakapotambuliwa , lakini  hadi  sasa  watu  152  ndio wanaotambuliwa  kuwa  wameuwawa.

Wapiganaji  kutoka  kundi  la  al-Shabaab  nchini  Somalia  walivamia viunga  vya   chuo  hicho  kikuu  mjini  Garissa , kilometa  350 kaskazini  mashariki  ya  nairobi  Aprili  2 , na  kuwafyatulia  risasi wanafunzi.